MALABO : Ajali ya ndege yauwa 60 Eaqutorial Guinea
18 Julai 2005Matangazo
Watu 60 wameuwawa wakati ndege iliotengenezwa Russia aina ya Anatov ilipoanguka na kuteketea nchini Equatorial Guinea muda mfupi baada ya kuruka kutoka mji mkuu wa Malabo.
Katika ujumbe wa radio kwa taifa hapo jana Rais Teodoro Obiang Ngwema ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia kuanguka kwa ndege hiyo hapo Jumamosi ambapo amesema imeuwa vijana wengi na wanawake wa Equatorial Guinea.
Radio ya taifa ilitangaza mapema huku ikipiga muziki wa kuzuhunisha kwamba ndege hiyo ilioanguka ikiwa kwenye safari ya ndani ya nchi katika kichaka kizito imeteketea kabisa,imeunguwa na kwamba hakuna mtu aliyenusurika.