Makala ya Sura ya Ujerumani safari hii inajikita kuhusu shughuli za makundi ya kihalifu kutoka Nigeria nchini Ujerumani pamoja na mikakati iliyopo kuyapiga vita makundi hayo. Makala hii imeandaliwa na Jan-Philipp Scholz na Andrea Lueg na msimulizi wako ni mimi Harrison Mwilima wa DW Berlin.