1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano yafikiwa Somalia kuhusu uchaguzi uliocheleweshwa

26 Mei 2021

Waziri wa kigeni Somalia Mohamed Abdirizak ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa makubaliano yamefikiwa kati ya serikali kuu na serikali za mikoa kuandaa uchaguzi wa kitaifa uliocheleweshwa kwa muda mrefu

https://p.dw.com/p/3tymY
Somalia Präsident Mohamed Abdullahi Mohamed | Farmajo
Picha: Str/AFP

Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Somalia Mohammed Abdirizak amesema makubaliano kuhusu masuala matatu muhimu ya kukamilisha mkataba huo yamefikiwa kimsingi jana, kufuatia kuhitimishwa kwa mazungumzo yaliyoanza Mei 22 kati ya serikali ya shirikisho na majimbo.

soma zaidi: Bunge la Somalia labatilisha nyongeza ya muhula wa Rais

Amesema tamko linaloeleza kwa kina makubaliano hayo litatolewa Alhamisi katika hafla ya kuhitimishwa rasmi.

Kumekuwa na shinikizo kubwa dhidi ya Rais Mohamed Abdullahi Mohamed baada ya uchaguzi uliopangwa Februari nane kushindwa kufanyika kwa sababu ya kukosekana kwa makubaliano ya jinsi uchaguzi huo unapaswa kuandaliwa.