1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUreno

Makasisi wa Katoliki Ureno waliwadhulumu kingono watoto 4815

13 Februari 2023

Viongozi wa kidini wa kanisa Katoliki nchini Ureno wamewadhulumu kingono watoto wasiopungua 4,815 kwa miaka 70 iliyopita yaani tangu mwaka 1950.

https://p.dw.com/p/4NQkc
Portugal | Kirche in Lissabon
Picha: Pedro Nunes/REUTERS

Ni kulingana na ripoti ya uchunguzi huru uliofanywa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita na matokeo yake kutangazwa leo ikikusanya ushuhuda kutoka kwa mamia ya waathiriwa wa manyanyaso hayo.

Wakati wa kutangazwa ripoti hiyo, Pedro Strecht, daktari bingwa wa matatizo ya akili hasa kwa watoto amewaambia waandishi wa habari mjini Lisbon kwamba ushuhuda waliokusanya unawawezesha kutambua mtandao mkubwa wa waathiriwa.

Stretcht amesema asilimia 77 ya waliohusika na  manyanyaso  hayo walikuwa wakuu wa mabaraza ya maaskofu, na waathiriwa wengi walikuwa wanaume.

Ameongeza kuwa waathiriwa walidhulumiwa katika shule za kikatoliki, katika nyumba za makasisi na kwenye makongamano miongoni mwa maeneo mengine.

Jose Ornelas, mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini humo alihudhuria kuzinduliwa kwa ripoti hiyo na atatoa kauli yake baadaye.