1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Glas alazwa hospitalini baada ya kukamatwa na polisi Equador

9 Aprili 2024

Makamu wa zamani wa rais wa Equador Jorge Glas, aliyekamatwa katika uvamizi wa ubalozi wa Mexico siku ya Ijumaa, amelazwa hospitalini baada ya kukataa kula.

https://p.dw.com/p/4eZoB
Jorge Glas
Makamu wa zamani wa rais wa Equador Jorge GlasPicha: Dolores Ochoa/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa mamlaka ya magereza nchini humo, Glas, mwenye umri wa miaka 54, anaendelea na matibabu kwenye hospitali ya jeshi la wanamaji mjini Guayaquil.

Polisi inadai kuwa Glas, anayetuhumiwa kwa ufisadi, alizimia kwa makusudi baada ya kumeza vidonge vya kukabiliana na mfadhaiko. 

Vyombo vya usalama vya Equador vilivamia ubalozi wa Mexico na kumkamata makamu huyo wa zamani wa rais, saa chache baada ya kupatiwa hifadhi ya kisiasa. Hatua iliyoibua mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo. 

Mapema Jumatatu mwanasheria wa Glas aliliambia shirika la habari la AFP kwamba anahofia usalama wa maisha ya mteja wake, na kuomba msaada wa kimataifa.