You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Kauli ya Papa Francis yazua hisia mseto
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema katika mahojiano kwamba Ukraine inapaswa kuwa na kile alichokiita ujasiri wa kupeperusha "bendera nyeupe" kama ishara ya kusalimu amri na kukubali kufanya mazungumzo ya kumaliza vita na Urusi. Kauli hiyo imeichukiza mno Ukraine na washirika wake wa Magharibi.
Madhara ya kiafya kwa madereva wa bodaboda
Makala ya afya yako Deo Kaji Makomba kutoka makao makuu ya Tanzania, Dodoma, anaangazia madhara ya kiafya wanayoweza kuyapata madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda ambao hujishughulisha na shughuli za usafirishaji abiria katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Usiweke simu yako kwenye mchele mkavu
Katika Sema Uvume wiki hii Suleman Mwiru anatizama tahadhari iliyotolewa na kampuni ya Apple juu ya tabia ya kuziweka simu kwenye mchele mkavu pindi zinapodondoka kwenye maji, badala yake fanya yafuatayo.
Zitto Kabwe amekiachaje chama cha ACT-Wazalendo ?
Silikiza mahojiano ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania Zitto Kabwe na George Njogopa wa DW-Kiswahili kwenye Kinagaubaga.
Somalia yajiunga rasmi na EAC
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeikaribisha rasmi Somalia kuwa mwanachama wake mpya.
Kaiko Njike: Waasi bado wanatatiza raia mashariki ya Kongo
Sudi Mnette anazungumza na Kanali Kaiko Njike, msemaji wa jeshi la Kongo linalopambana na waasi mashariki ya nchi hiyo.
Mastaa wageuka ombaomba mitandaoni?
Ni jambo la kawaida kuona ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa mastaa wakiomba msaada wa kifedha kutoka kwa mashabiki wao na wafuasi wao. Iwe ni kwa ajili ya kulipa bili za matibabu, kulipa kodi za nyumba au hata kununua kitu cha thamani. Bruce Amani anaimulika mada hii katika Vijana mchakamchaka.
Ukraine inataka kuungwa mkono na Waafrika
Ukraine inatafuta uungwaji mkono kutoka katika pande tofauti za ulimwengu kufuatia vita vyake a Urusi. Hivi karibuni ili kulifanyika kongamano la kimataifa kuhusu vita hivyo lililofahamika kama Cafe Kyiv, mwandishi wa habari Issac Amuke kutoka Kenya alikuwa mwana jopo katika kongamano hilo lililofanyika Februari 2024. Zaidi msikilize alipozugumza na Sudi Mnette.
Juhudi za serikali ya Kenya kuzalisha dawa zake yenyewe
Ungana na Wakio Mbogho, Ripota wa DW mjini Nakuru, Kenya, katika Makala ya Afya Yako inayomulika jitihada za taifa la Kenya kustawisha uzalishaji wa dawa na bidhaa za matibabu nchini humo.
Biteko:Uhakika mgao wa umeme mwisho Machi Tanzania
Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania, Dotto Biteko amesema taarifa ya kuufikisha mwisho kwa mgao wa umeme Tanzania mwezi Machi.
Faida za Misitu kusini mwa Tanzania
Katika Makala hii ya Mtu na Mazingira Salma Mkalibala anaangazia, faida za kimazingira zinazotokana na uwepo wa Misitu ya Ukanda wa Pwani na changamoto zake.
Je umeshawahi kuwa kwenye mahusiano na mtu aliyekuzidi umri?
Kuna mitazamo tofauti juu ya vijana wanaojihusisha na uhusiano wa kimapenzi na watu waliowazidi umri. Lakini vipi mahusiano hayo yanapogeuka kuwa ya kusaka maslahi? Suleiman Mwiru anakueleza zaidi katika Makala hii.
Vijana Mchakamchaka: Je, unaitumiaje simu yako?
Je, wewe unaitumiaje simu yako? Ungana na Selina Mdemu akizungumzia matumizi ya simu kwa vijana.
Wimbi la rekodi za dunia za Guinness
Katika Makala hii ya vijana mchakamchaka, tunafahamu zaidi kuhusu rekodi za dunia, za Guinness. Je, ni za kujipatia sifa tu? Au zinakuza maadili ya kijamii na kuhamasisha jamii kuhusu masuala muhimu? Ni rekodi ipi ambayo ungependa iandikwe?
Mazingira: Ujasiriamali kupitia ukusanyaji taka Kisumu
Ongezeko la idadi ya watu linamaanisha ongezeko pia la takataka zinazotokana na shughuli zinazofanywa na watu hao.
Kujiuzulu kwa Rais wa Hungary K. Novak
Jumamosi ya Februari 10, 2024- Rais wa Hungary Katalin Novak alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu kufuatia uamuzi wa kutoa msamaha kwa mtu aliyekuwa jela kwa kosa la kukutwa na hatia ya kuficha taarifa muhimu kwenye kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto. Katika kipindi cha Mwangaza wa Ulaya, tunaangazia sakata hili lililomfanya Rais Novak, rais wa kwanza mwanake wa Hungary kujiuzulu.
Unapendelea kocha wa Kiafrika au wa kigeni?
“Kama makocha wa Kiafrika watapewa raslimali za kutosha na uhuru wa kufanya kazi yao bila uingiliwaji, hakuna timu ya taifa barani Afrika itahitaji kocha wa kigeni.“ Unakubaliana na hii? Hiyo ndio mada yetu katika Vijana Mubashara.
Wimbii la migomo: Ujerumani yakabiliwa na mkwamo
Mwaka mpya ulianza kwa wimbi la migomo nchini Ujerumani. je, Wajerumani wanagoma zaidi hivi sasa kuliko hapo kabla na je, nchi hiyo inakabiliwa na tishio la hali kama ya nchini Ubelgiji au Ufaransa?
Sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania. Sikiliza mjadala huo.
Madhara ya kusitisha ufadhili kwa UNRWA
Mohammed Khelef anachambua athari mbaya za uamuzi wa kusitisha ufadhili kwa shirika la UNRWA.
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya CCM
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya tangu kuzaliwa kwa CCM, chama tawala cha Tanzania.
Mwangaza wa Ulaya: Ulaya imejiandaaje kwa kurejea utawala wa Donald Trump?
Wakati kampeni za urais nchini Marekani zikiashiria uwezekano wa kurudiwa kwa mchuano kati ya Donald Trump na Joe Biden, Ulaya inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa. Siyo tu kura za uchunguzi wa maoni zinazompa Trump nafasi halisi ya kurejea Ikulu ya White House. Gazeti la New York Times liliripoti kuwa viongozi wengi wa dunia wanaamini Trump anarudi kwa muhula wa pili. Zaidi katika Mwangaza wa Ulaya.
Makala ya Karibuni ya Februari 3, 2024
Mwanamke wa Thailand ameshtakiwa kwa kupatikana na mtoto wa simba kinyume cha sheria.
Kinagaubaga: Mwelekeo wa soka nchini Tanzania
Kocha Matola : Soka la Tanzania bado lina changamoto kubwa. Tanzania ilifungwa mechi moja na kutoka sare mbili AFCON.
Upopulisti, mitandao na demokrasia
Baruani Mshale anafafanua jinsi upopulisti unavyoshika kasi barani Afrika na jinsi zilivyo hatari kwa demokrasia.
Kinagaubaga: Kenya, Tanzania na Uganda kuandaa AFCON 2027
Rais wa shirikisho la soka la mpira wa mguu Tanzania TFF Wallace Karia aelezea nafasi ya Tanzania AFCON 2027.
Kinagaubaga: Mwamko wa kibiashara visiwani Zanzibar
Upi mwelekeo wa sekta ya biashara visiwani Zanzibar? Waziri mwenye dhamana Omar Said Shaban anaeleza kwenye Kinagaubaga.
Kinagaubaga: DP World yazidi kukosolewa Tanzania
Mjadala wa ubinafsishaji wa Bandari kuu ya Dar es Salaam kwa kampuni ya Dubai ya DP world umezusha wasiwasi kwa raia wa taifa hilo na kuanza kuwagawa watu kwa itikadi na maeneo wanayotokea.
Ugunduzi wa aina mpya ya Mbu na kitisho cha Malaria Kenya
Taasisi ya utafiti wa matibabu KEMRI imegundua aina mpya ya mbu nchini Kenya na imetoa tahadhari juu ya mbu hao hatari.
Vijana Mchakamchaka: Mtindo wa upigaji picha za kuvutia
Vijana Mubashara inaangazia umuhimu wa kupiga picha na jinsi vijana wa kileo walivyobadilisha tasnia ya upigaji picha.
Vijana Mchakamchaka: Nidhamu ya kufanya mazoezi
Sio wote wanaofanya mazoezi wana nia ya kujenga mwili. Vijana Mchakamchaka leo inaangazia sababu za vijana kuingia gym.
Vijana Mubashara: Sababu zinazokufanya usifikie malengo yako
Miongoni mwa sababu za mtu kutofikia malengo yake ni kupishana kiimani, kutilia mashaka uweko wako na kukatishwa tamaa.
Mbiu ya Mnyonge: Askari polisi na vitendo vya kikatili
Raia anatakiwa ajihisi yuko salama zaidi mbele ya maafisa wa polisi, lakini katika matukio kadhaa inakuwa kinyume chake.
Jinsi Kiswahili kinavyotumika Oman
Salma Said anasimulia jinsi lugha ya Kiswahili ilivyoshamiri nchini Oman.
Wanawake na Maendeleo: Chakula cha Kiswahili maarufu Oman
Salma Said anazugumzia jinsi utamaduni wa Waswahili unavyodumishwa nchini Oman kupitia mapishi na vyakula.
Afya Yako: Umuhimu wa kufanya vipimo mara kwa mara
Kwenye Afya Yako leo, Selina Mdemu anazungumzia umuhimu wa kufanya vipimo vya mwili mara kwa mara ili kuchunga afya.
Dunia Yetu Leo Mchana Januari 20, 2024
Sikiliza Matangazo ya Mchana Januari 20, 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Uteuzi wa Gabriel Attal kama Waziri Mkuu wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimteua Januari 9 mwaka 2024, Gabriel Attal kuwa Waziri Mkuu mpya. Attal mwenye umri wa miaka 34 anachukua nafasi ya Elisabeth Borne aliyejiuzulu sambamba na serikali aliyokuwa akiiongoza. Hatua hii ya Macron inachukuliwa kama ya kimkakati na yenye lengo la kuisafisha serikali yake ambayo imekuwa ikikabiliwa na kashfa mbalimbali.
Vijana na Uongozi: Ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano
Kwenye Makala ya Vijana na Uongozi, utamsikia Maxence Melo, mmiliki wa Jukwaa la Jamii Forums nchini Tanzania akizungumzia masuala mbalimbali kuanzia hatua zilizopigwa kwenye eneo zima la ukuaji wa sekta ya teknolojia na mitandao ya kijamii iliyorahisha pakubwa mawasiliano. Ana mengi ya kukueleza msikilizaji. Tafadhali ungana naye hapa anapozungumza na mwenzetu Anuary Mkama.
Kinagaubaga: Lazima wakazi wote waondoke Ngorongoro
Mpango wa kuwahamisha jamii ya wamasai katika Hifadhi ya Ngorongoro Tanzania, umeendelea kukabiliwa na ukosoaji huku, makundi ya watetezi yakilalamika kuwa serikali inazuia huduma muhimu kwa lengo la kuwashinikiza waondoke.
Mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza mafuta ya dizeli
Hussen Ndekeja ni kijana wa kitanzania mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza mafuta ya dizeli kwa kutumia taka za plastiki zinazokusanywa katika mazingira mbalimbali. Kupitia ubunifu huo amepata nafasi ya kuwafundisha vijana wenzake ambao waliibuka washindi katika mashindano ya ubunifu kwa vijana,yalioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania.
Makala ya Karibuni na dhana ya kufunga mvua Tanzania
Katika kipindi hiki cha Karibuni utamsikia msikilizaji wa mwezi Kamalos Kisando wa Butembo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Na kwenye Sadiki Ukipenda kuna dhana ya kufunga mvua ya huko kusini mwa Tanzania.
Kinagaubaga - Hatma ya ACT Wazalendo serikali ya Zanzibar
Sudi Mnette amezungumza na mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo kuhusu hatma yao ndani ya serikali ya Zanzibar.
Meza ya Duara - Je, ulimwengu umeshindwa kumaliza migogoro?
Zainab Aziz amewaalika wachambuzi wa siasa za kimataifa kwenye kipindi cha Maoni mbele ya meza ya duara kuhusu migogoro.
Je, mataifa ya Magharibi yanaweza kuchukua hatua gani zaidi dhidi ya Urusi?
Wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukikaribia kutimiza miaka miwili, mataifa ya magharibi yamekuwa yakitatizika juu ya mbinu gani wazitumie ili kukabiliana na Moscow. Marekani na washirika wake wa Magharibi wamekuwa wakizidisha vikwazo dhidi ya Urusi lakini vimeonekana kutofikia jumla ya malengo yake. Ungana na Bakari Ubena katika kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya kufahamu turufu zilizosalia.
Kinagaubaga: Tanzania kuwaadhibu wanaotumia vibaya mitandao
Baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dokta Philip Mpango kujitokeza hadharani baada ya taribani mwezi mmoja na kuonesha kusikitishwa kwake kwa kuzushiwa kifo mitandaoni. Waziri wa Habari wa Tanzania, Nape Nnauye aliziagiza mamlaka kufanya uchunguzi kwa wote waliosambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii. Sudi Mnette alizungumza nae.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 3
Ukurasa unaofuatia