1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maji yapungua Cyprus

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cmxp

NICOSIA:

Ukame unaochokikumba kisiwa cha Cyprus unakiweka katika hali ya kuagiza nje maji ili kukidhi mahitaji ya maji yanayopungua kila siku kutokana na kukauka kwa matanki ya kuhifadhi maji.

Wakuu wanafikiria kuagiza maji kutoka kisiwa cha Ugiriki cha Crete ikiwa ukame utaongezeka.Ukosefu wa maji umelazimisha mgao wa maji kwa wakulima na mgao pia unaweza ukalazimishwa kwa kila nyumba ikiwa hali haitarekebika ifikapo mwezi wa Aprili.Duru za kiserikali zaonyesha kuwa kiwango cha mvua nchini Cyprus kimepungua kwa asili mia 20 kwa kipindi cha miaka 35 iliopita,wakisema hali hiyo ni athari za kubadilika kwa hali ya hewa.