Maji na Nishati: Siasa za Mabwawa
Ulimwenguni kote, mabwawa makubwa yanaweza kukuza uchumi na kutumiwa kama ishara ya hadhi na mamlaka. Lakini nini kinatokea kwa jamii zilizoko chini ya mabwawa hayo?
GERD: Alama ya ufahari
Likiwa na urefu wa mita 145 na karibu kilomita 2, Bwawa la 5GW Grand Ethiopian Renaissance linatarajiwa kuongeza maradufu uzalishaji wa umeme nchini humo. Bila ya kukubaliana na nchi zilizoko chini ya bwawa hilo, Ethiopia iliujenga kwa ufadhili binafsi na serikali baada ya Benki ya Dunia kukataa kuufadhili. Sasa umekuwa chanzo kikubwa zaidi cha nishati na fahari ya kitaifa nchini Ethiopia.
Maisha kwenye Nile
Misri na Sudan zinahofia matokeo ya GERD. Ethiopia itakuwa na udhibiti wa maji ambayo wanayategemea kumwagilia mashamba katika eneo la Nile Delta. Ili kuzalisha umeme, maji yanatakiwa kuendelea kutiririka, lakini majirani zake hawajashawishika na hakikisho la Ethiopia kwamba haitalitumia bwawa hilo kumwagilia na hasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotishia kupunguza maji.
Mabwawa kwenye mto Mekong
Tangu miaka ya 1990, China imejenga mabwawa makubwa 11 kwenye Mto Mekong, yanayoifanya kuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa nishati itokanayo na maji duniani - chanzo chake cha pili kikubwa cha umeme baada ya makaa ya mawe. Lakini pamoja na Laos, Thailand, Vietnam na Cambodia ambazo zote zinategemea Mekong, ujenzi huu umesababisha mashaka kwa mataifa yaliyo chini ya mabwawa hayo.
Ukame nchini Cambodia
Mto Mekong umekuwa ukikabiliwa na msukusuko na hasa wakati mabwawa ya China yanapokumbwa na mabadiliko ya mtiririko wa maji yake. Ukame umeongezeka, hifadhi ya samaki imeathirika, na pia kuathiri pakubwa jumuiya za wavuvi na wakulima nchini Thailand na Cambodia, ingawa data za satelaiti zimeonyesha wastani wa juu wa kuyeyuka theluji pamoja na mvua na kuongeza maji sehemu ya mto iliyoko China.
Kujitanua kwa China kimataifa katika miradi ya umeme wa maji
China pia inawekeza katika mamia ya miradi ya umeme wa maji nje ya nchi, kutoka Laos hadi Ureno, Kazakhstan hadi Argentina na kote Afrika - ikiwa ni pamoja na bwawa la Souapiti nchini Guinea. Hapo awali, miradi hii mikubwa ya miundombinu ilifadhiliwa na Benki ya Dunia, lakini sasa China inajiimarisha na kuwa mfadhili mkuu na haihitaji makubaliano kutoka kwa nchi zinazotumia mito kwa ushirikiano.
Wengine wameyahama makazi yao
Bwawa la Souapiti nchini Guinea, linalofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maji na Umeme la China, litazalisha umeme wa megawati 450 katika nchi ambayo hata hivyo ni wachache tu wanaopata umeme wa kuaminika. Lakini ili kufanikisha kuwa na hifadhi kubwa zaidi itakayohitaji kilomita za mraba 253 za ardhi, watu 16,000 kutoka zaidi ya vijiji 100 wameyahama makazi yao kulingana na Human Rights Watch.
Kuunganisha mipaka?
Bwawa la Itaipu kwenye Mto Paraná kati ya Brazil na Paraguay ni mojawapo ya maporomoko ya maji yanayovutia zaidi ulimwenguni na yamewakosesha makazi watu 65,000. Pia lilisababisha mvutano kati ya nchi hizo mbili zilizotia saini makubaliano ya kushirikiana katika mradi wa umeme wa maji yanayoumiliki tangu mwaka 1973. Lakini kwa kuwa kiwango cha juu cha kinakwenda Brazil, bwawa hilo bado lina utata.
Kuubadilisha mto Colorado
Mpaka huu wa Mexico na Marekani huleta tu picha za uhamiaji na ndoto ya Trump ya kujenga ukuta kuzigawa nchi hizo. Lakini pamoja na mvutano juu ya watu wanaokimbilia eneo la kaskazini kumekuwa na mashaka juu ya maji yanayotokea Mto Colorado na kushika mwelekeo tofauti. Mto huo hupitia majimbo saba ya Marekani na mabwawa mengi ukielekea Mexico, ambayo maji yake humwagilia mazao ya Marekani.
Kumwagilia Bonde la Mexicali
Lakini nchi hizo mbili zimekuwa zikishirikiana kutumia Bwawa la Morelos kwenye mpaka wao wa pamoja kumwagilia Bonde la Mexicali lenye mfumo wa "pulse" unaofanana na mtiririko wa asili katika bwawa la Colorado. Mtaalamu wa siasa za maji Scott Moore anasema hii inaonyesha "ushirikiano kati ya Marekani na Mexico lakini pia kati ya watetezi wa mazingira, wakulima na wasimamizi wa ikolojia."