1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Ujerumani Kongo na waziri mkuu mpya Poland.

Ramadhan Ali11 Julai 2006

vikosi vya Ujerumani vilivyopelekwa Kongo kusimamia uchaguzi na rais wa Poland kumteua nduguye-pacha kuunda serikali mpya ni mada zilizotia fora katika safu za leo za wahariri wa magazeti ya Ujerumani:

https://p.dw.com/p/CHVZ

Tukianzia na vikosi vya Ujerumani vya askari 2000 vilivyopelekwa Kongo kusimamia uchaguzi ujao,gazeti la BERLINER ZEITUNG linaukosoa msimamo wa Umoja wa ulaya uliotuma vikosi hivyo kuwa ni wa kigeu-geu.

Gazeti laandika kwa tabia hiyo ya kusitasita, UU unahatarisha mafanikio ya matumizi ya jeshi hilo.Kwani UU unaegemea zaidi kuwa jeshi la kutishia tu,lakini pakizuka kweli fujo,wapigajikura katika sehemu mbali mbali za Kongo wakizuiliwa kutia kura zao, vikosi hivyo vya kimataifa vitakabiliwa na mtihani.Na hapo tena UU utapaswa kutuma huko vikosi zaidi na muda wao wa kukaa Kongo utakuwa mrefu zaidi kuliko ilivyopangwa miezi 4 tu.Kwamba UU hautuhubutu kusema hayo wazi ,haichangii kuonesha unajiaamini.” Ni ucahmbuzi wa Berliner zeitung.

Ama gazeti la kibiashara la HANDELSBLATT linalo chapishwa mjini Düsseldorf linadai ni bora kuwaambia wanajeshi ukweli zaidi wa hali ya mambo.Kuwaambia tangu mwanzo kabisa wa jukumu lao lini itakua mwisho wa jukumu hilo ni kujifanya mjuaji.Ni bora hivyo ukichukulia wanaweza wanajeshi hao kubidi kutumiwa nchini Sudan.Hakuna anaeweza kuondoa leo uwezekanao kwmba waziri wa ulinzi hatabidi kuchukua mti wa X-masi kwenda nao Afrika …”

Kwa maoni ya gazeti la OSTSEE-ZEITUNG kutoka Rostock, hatari za kupelekwa majeshi ya Ujerumani nchini Kongo ni kubwa zaidi kuliko faida zake.

Linaandika kwamba, pasitarajiwe maajabu kutokana ujumbe huu .Kuwapo kwa wanajeshi Kongo ni alama tu kuwa jamii ya kimataifa haitaki kuiachia nchi hii yenye utajiri mkubwa wa mali-asili kutumbikia zaidi katika machafuko….Zitaka zaidi kuona chama kilichoshindwa kinaridhia kushindwa.

Nalo gazeti la ESSLINGER ZEITUNG linakosoa kuwekwa sehemu kubwa ya askari wa ujerumani katika ardhi ya nchi jirani ya Gabun.Kwani, linasema gazeti, katika mji mkuu wa Kongo-Kinshasa, ni askari 200 tu waliopagwa kuwekwa.Kuzunguka kushika zamu si sehemu ya mpango wao.Kwa njia hii kuwapo nchini kwa wanajeshi wa ujerumani hakutambuliki.Kwa njia hii haitawezekana kuwatishia wale wanaopanga kuzusha fujo wala kuwalinda wapendao amani.

Likitugeuzia mada gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND linachambua kisa cha ndugu-wawili-pacha nchini Poland Lech na Jaroslaw Kaczynski kushika hatamu za kuiongoza Poland.

Lech ndie rais na amemteua nduguye Jaroslaw kuunda serikali mpya baada ya waziri-mkuu Marcinkiewicz kujiuzulu.

Gazeti laandika:

Mabadiliko haya ya waziri-mkuu yana jambo moja jema:

Kwani, lasema gazeti,Poland na ulimwengu inajua sasa Poland inatawaliwa na nani ?

Siasa nchini Poland inaongozwa na ndugu-wawili-mapacha wenye msimamo wa kizalendo wakihafidhina.Wana msimamo wakutosahau yaliopita mbele ya Ujerumani na wa kufuata njia yao pekee kando na Umoja wa Ulaya.

Likitumalizia gameti la STUTTGARTER ZEITUNG lakumbusha:

“Seriali ya poland tangu iliposhika madaraka mwishoni mwa m waka uliopita imechochea balaa jingi na UU.Katika maswali yak odi-ziyada,kutaifisha mabenki,bomba la ma futa baina ya Urusi na Ujerumani,katiba ya Ulaya,sarafu ya Euro…..na kadhalika.Wanasiasa wa Poland lashasuri gazeti,wanapaswa kujua wanakata kwa msumeno miguu ya kiti wanachokikalia.