Majeshi ya Ujerumani Afghanistan
30 Januari 2008Mada ya usoni katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo ni dai la NATO kuwa Ujerumani ipeleke wanajeshi wake kupigana nchini Afghanistan.Serikali ya Ujerumani mjini Berlin inazingatia kupitisha uamuzi wake hivi karibuni.Tayari lakini hivi sasa kuna maoni yaliotanda kwamba Ujerumani haiwezi kukataa kuitikia mwito huo.
Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG linalochapishwa Frankfurt/Order laandika:
"Sasa hakuna tena mchezo kwa Bundeswehr-jeshi la Ujerumani:Kwa ombi rasmi kutoka NATO-shirika la ulinzi la magharibi kwa Ujerumani kuchangia vikosi vya kupigana,siku inajongelea siku ya kutuma wanajeshi wake kupöigana nchini Afghanistan.Hii maana yake sura mpya inachomoza,kwani kuchangia Ujerumani majeshi yake huko hindukuch kunachokua sura ya hatari kabisa na hii licha ya majaribio yote kwa wanasiasa wa serikali ya muungano ya Ujerumani kuzima hatari zake."
Hayo yalikua maoni ya MÄRKISCHE ODERZEITUNG.
Gazeti la Frankfurter Allgemeine linakosoa kusitasita kwa serikali ya Ujerumani kukiita kwa jina kile hasa kinachotokea hapa:Laandika:
"Hatua ya kutuma majeshi kupigana ni barabara na inaegemea sababu za kuonesha umoja na mshikamano na NATo na ni hatua iliokua ichukuliwe zamani.hatahivyo,wizara ya ulinzi inapata taabu kwa mara nyengine tena uamuzi ambao kindani ndani zamani umepitishwa kuuweka bayana hadharani kwa umma unaokosoa mchango wa aina hiyo."
Ama gazeti la LANDESZEITUNG linalochapishwa mjini Lüneburg laandika:
"Serikali ya muungano wa vyama viwili vikuu imo kwenye kizungumkuti ikikwepa kutaja "majeshi ya kupigana".
Yamkini matumizi ya kikosi cha kupigana kisheria yalingana na jukumu la vikosi vya ISAF,kisiasa lakini ,hayana wafuasi.....Kuna sababu kuungamkono matumizi ya jeshi la Ujerumani wazi wazi na bila kigeugeu.Ndio Bundesweher-jeshi la Ujerumani haliwezi kulazimisha amani kwa nguvu za mtutu wa bunduki,
Lakini kwa Bundeswehr-jeshi la Ujerumani jukumu la kwenda vitani ni jukumu la kupigana vita."
Gazeti la TAGESSPIEGEL linalochapishwa mjini Berlin, daima likielewa kwamba kutuma majeshi nchini Afghanistan ni hatari.Na sio tu kutokana na kitisho cha kushambuliwa.Na yule anaepeleka askari wake huko,anaelewa timamu atabidi kupigana. Na yule anaetarajia kupigana laendelea gazeti:
"Anategemea kuwa na majeruhi na maiti.Kusema wazi na kinaganaga hakuna akijua wazi athari zake aliewaambia hayo wananchi kwamba inabidi kuilinda Ujerumani kwa kupigana huko Hindukuch."
Mod: gazeti la kusini mwa Ujerumani-Stuttgarter Zeitung linashughulikia matumaini ya kufanikiwa kwa ujumbe iliobeba Ujerumani nchini Afghanistan.Laandika:
"Umma wa Afghanistan baada ya robo-karne ya vita vya kienyeji una shaka shaka na azma za kambi ya magharibi,hata hivyo, hauoneshi uadui.Nafasi za za kusimamisha usalama katika nchi hii muda mrefu ujao si mbaya.Zinabidi kujumuisha mkakati wa kijeshi kwavile wataliban hawatatoweka.Pia Afghanistan itahitaji kiinuamgongo cha kunyanyua maisha ya raia."
Na mwishoe, gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaimurika wazi hali inayojikuta shirika la ulinzi la NATO:
" hakuna shaka,hili ni jukulu lenye hatari iliojitwika.Ni jukumu ambalo tangu miaka 2 iliopita linatekelezwa na vikosi vya N orway.Ni jukumu ambalo hakuna mshirika mwengine wa NATO aliejitolea kulibeba.Na sio tu kwa kuwa ni jukumu lenye hatari,bali kwa kuwa shirika la ulinzi la NATO limefikia kikomo cha uwezo wake nchini Afghanistan.
Ujerumani kwahivyo, haina chaguo jengine bali kuubeba mzigo iliopewa."