1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Iraq bado yanapambana na wanamgambo wa al-Sadr.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVes

Basra.

Majeshi ya serikali yameendelea kupambana na wanamgambo wa jeshi la Mahdi katika mji wa bandari wa Basra.

Kiasi cha watu 40 wameripotiwa kuuwawa katika mapigano na wengine 200 wamejeruhiwa.

Wanamgambo wa Kishia yanaomuunga mkono kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr pia wameshambulia wanajeshi wa Marekani mjini Baghdad pamoja na miji mingine inayoshikiliwa na Washia.

Makombora yalishambulia eneo lenye ulinzi mkali la mji wa Baghdad linalojulikana kama ukanda wa kijani na kuwajeruhi watu kadha. Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki , ambaye hivi sasa anaangalia operesheni hiyo ya kurejesha amani katika mji wa Basra, amewataka wanamgambo hao wa Kishia kuweka silaha zao chini katika muda wa saa 72 ama watakabiliwa na adhabu kali.

Akijibu tamko hilo, akiongozi wa jeshi hilo al-Sadr amedai kuwa al-Maliki aondoke mjini Basra na kuanza majadiliano.