1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Majeshi ya Armenia na Azerbaijan yapambana mpakani

12 Aprili 2023

Vikosi vya kijeshi vya Armenia na Azerbaijan, jana vilikabiliana katika mpaka wao wa pamoja na kusababaisha vifo vya takriban wanajeshi saba.

https://p.dw.com/p/4Pwh5
Vituo vya ukaguzi kwenye mpaka wa Armenia na Azerbaijan
Armenia na Azerbaijan zimetumbukia kwenye uhasama kwa zaidi ya miongo mitatu. Picha: Gilles Bader/ZUMAPRESS/picture alliance

Haya ni kulingana na wizara za ulinzi za mataifa hayo mawili.

Wizara ya ulinzi ya Armenia, imesema kuwa wanajeshi wa Azerbaijan waliwafyatulia risasi wanajeshi wake waliokuwa wakifanya kazi ya uhandisi ambayo haikutajwa karibu na mji wa Armenia wa Tegh ulio umbali wa kilomita 3 kutoka mpakani.

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa wanajeshi wanne wa Armenia waliuawa na sita kujeruhiwa.

Azerbaijan nayo imesema kuwa ni wanajeshi wa Armenia waliofyetua risasi na kusababisha vifo vya wanajeshi wake watatu.

Makabiliano hayo yanafuatia miezi kadhaa ya mvutano kuhusu kufungwa kwa barabara ya pekee inayoiunganisha Armenia na jimbo la Nagorno-Karabakh lililo ndani ya Azerbaijan lakini lenye wakaazi wengi wa Kiarmenia.