1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeruhi wa mji wa Qusayr wachapa mguu kuelekea Lebanon

13 Juni 2013

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria, wanasema hali ya maelfu ya watu majeruhui katika mji wa Qusayr ni mbaya zaidi na hadi sasa bado wapo katika mji huo.Umoja wa Mataifa umeomba huduma zipelekwe haraka katika

https://p.dw.com/p/18ozL
Mji wa Qusayr nchini Syria
Mji wa Qusayr nchini SyriaPicha: STR/AFP/Getty Images

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria, wanasema hali ya maelfu ya watu majeruhui katika mji wa Qusayr ni mbaya zaidi na hadi sasa bado wapo katika mji huo.Umoja wa Mataifa umeomba huduma za kiutu zipelekwe haraka katika mji huo.

Licha ya mchoko wa siku tano za matembezi kuelekea eneo salama nchini Lebanon akivuka milima na mabonbde, raia wa Syria aliejitambulisha kwa jina la Mohammed kwa kuhofia usalama wake, alilaazimika kutembea licha ya kuwa na majeraha katika mguu wake, huku akijificha asionekane na vikosi vya serikali.

Mohamed mwenye umri wa miaka 35 alijeruhiwa katika mashambulizi ya mji wa Qusayr, na sasa anatibwa katika hospitali ya kienyeji mjini Minieh kasikazini mwa Lebanon, baada ya vikosi vya Syria, vikisaidiwa na Hezbollah kuchukua udhibiti katika mji wake juma lililopita.

Mwandishi wa shirika la habari la AFP aliombwa kutotaja njia walioichukuwa wakimbizi kufika nchini Lebanon, wala kuuliza iwapo waliojeruhiwa ni raia wa kawaida au waasi. Mohammed alisema watu walijaribu kumuondoa mjini Qusayr kwa kutumia gari lakini kulikuwa na uharibifu mkubwa na hivyo gari halikuweza kuondoka.

Baada ya kukwama safari hiyo, waliamua kutembea kwa miguu hali ambayo ilipoteza kiasi chake kikubwa cha damu akiwa amevaa suruali moja na fulana, nguo ambazo amezivaa kwa muda wa siku tano mfululizo. Walipofika kijiji cha karibu na Qusayr ambacho hakutaka kutaja jina lake, yeye na baadhi ya majeruhi wengine walipatiwa huduma ya kwanza, lakini hakukuwa na damu ya kutosha kwa ajili ya kila mtu.

Qusayr yadhibitiwa na utawala wa Syria.

Na wakati jeshi la utawala wa Syria likiimarisha udhibiti wake katika mji wa Qusayr,uliokuwa chini ya udhibiti wa waasi mwaka mmoja, Mohammed na majeruhi wengine 30 waliamua kuhatarisha maisha yao kwa kuikimbia Syria kwa mguu kuelekea nchini Lebanon.

Askari wa utawala wa Syria
Askari wa utawala wa SyriaPicha: JOSEPH EID/AFP/Getty Images

Anasema walitembea kwa mguu kila siku usiku kwa muda wa siku tano na kupumzika muda wa mchana ili wasionwe na wanajeshi wa utawala wa Syria na kila wakiwaona askari, walikuwa wanajificha katika majani ya miti.

Watu hao waliokimbia nchini Syria kuelekea Lebanon, walikuwa na majeraha ya miguu,kichwani,mgongo na tumboni, na hawakuwa na dawa za kutuliza maumivu na hapo Mohammed alianza kutokwa na damu na kuwekwa bendeji katika majeraha yake kwa kutumia nguo za watu waliokuwa karibu yake.

Wakimbizi hao walipata ahueni baada ya kuchomoza jua siku ya Jumapili wakati walipofika kasikazini mwa mji wa Akkar nchini Lebanoni, na hapo wakahamishiwa katika Hospitali ya Minieh karibu na pwani ya bahari ya kati.

Katika safari hiyo, kulikuwa na Akram, mwenye umri wa miaka 40 ambaye naye alisafiri pamoja na Mohammad katika safari hiyo ya kukimbilia nchini Lebanon,akiwa amevaa fulana na suruari fupi ambayo alisaidiwa na watu wa hospitali.

Akram anakumbuka siku yalipotokea mabomu ya kutisha katika mji wa Qusayr, siku ambayo mji huo ulitekwa lakini zaidi anakumbuka siku ambayo walikosa hata dawa ya kutuliza maumivu ya majeraha yao katika hospitali ya kijijini iliokuwa imejaa wagonjwa.

Akram anakumbuka safari yake pamoja na Mohammed wakati walipokaa kwa muda wa saa 24 bila kula wala kupata maji , Kwani walifika nchini Lebanon saa 12:00 asubuhi siku ya jumapili.

Akiongea na shirika la habari la AFP Jumapili baada ya kuwasili majeruhi hao,Mkurugenzi wa Hospitali ya Miniel Amer Alameddine alisema baadhi ya majeruhi hao walikuwa hawawezi kujibu maswali ya Daktari kutokana na kujeruhiwa vibaya.

Abu Rael ambaye anasaidia wakimbizi wanaowasili kutoka kaskazini mwa Lebanon ameliambaia shirika la habari la AFP kuwa hospitali hiyo imekodishwa na wanaharakati kwa ajili ya kuwatibia watu wenye majeraha. Mashirika ya Lebanon yamekuwa yakiandaa mikate, chakula na hata magodoro kwa majeruhi hao.

Mwandishi:Hashimu Gulana/AFP

Mhariri: Ssessanga iddi