1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha mabomu chaibua wasiwasi Ujerumani

28 Oktoba 2023

Polisi walilazimika kwa mara nyingine kuchunguza vitisho kadhaa vya mabomu nchini Ujerumani jana Ijumaa huku watu wakiondolewa shuleni na kwenye majengo ya umma.

https://p.dw.com/p/4Y8Xk
Polisi akipita na mbwa katika shule ya msingi na sekondari ya Pulsnitz huko Saxony baada ya kupokea kitisho cha bomu
Polisi akipita na mbwa katika shule ya msingi na sekondari ya Pulsnitz huko Saxony baada ya kupokea kitisho cha bomuPicha: Rocci Klein/dpa/picture alliance

Majengo ya shule na baadhi ya taasisi za umma kote nchini Ujerumani kwa mara nyingine yalikumbwa na vitisho vya mabomu jana Ijumaa.

Wanafunzi waliondolewa katika baadhi ya shule baada ya kupata vitisho kupitia barua pepe. Ingawa haiko wazi visa hivi vinahusishwa na vita vya Israel huko Gaza na wengine wakiviunganisha na vita vya Ukraine.

Wizara ya mambo ya ndani ya ujerumani hata hivyo imesema hawana uhakika kama vitisho hivyo vinahusiana na itikadi kali vinginevyo na kuongeza kuwa inafanya uchunguzi, ingawa bado havijaonyesha kitisho kikubwa.

Siku ya Ijumaa shule mbili na jengo la halmashauri vilifungwa mashariki mwa Thuringia na wanafunzi waliondolewa kwenye karibu shule sita kusinimagharibi mwa Baden-Wurttemberg, moja katika jimbo la Bavaria na nyingine magharibi mwa North Rhine-Westphalia.