Maisha ya Helmut Kohl
Maisha ya Helmut Kohl
MAISHA YA HELMUT KOHL
Tarehe mosi Octoba Helmut kohl alichaguliwa kuwa kansela wa Ujerumani. Aliongoza nchi hiyo kwa miaka 16 ndie kansela aliyeingoza nch ya ujerumani kwa muda mrefu hadi sasa. Umaarufu mkubwa alioupata katika uongozi wake ni kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin ulisababisha kuungana kwa ujerumani ya mashariki na magharibi.1998 Kohl alijiuzulu kuwa kiongozi wa chama cha CDU.
Kupanda kwake kisiasa katika zama za Adenauer
Mwaka 1947 Helmut Kohl alijiunga na chama cha CDU na ni mwanzilishi wa Muungano vijana katika mji wake wa Ludwigshafen. Kutoka 1950, kwa mara ya kwanza alisoma sheria, basi historia na sayansi ya siasa. Wakati huo Kansela wa Ujerumani alikuwa ni Konrad Adenauer. Kohl alijifunza mengi kutoka kwake
Waziri Mkuu kijana
1966 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CDU katika Rhineland-Palatinate. 1969 aliteuliwa kuwa waziri mkuu na miaka miwili baadae alishinda kuwa Kansela wa Ujerumani.
Picha halisi ya familia yake
Wakati wa likizo Helmut Kohl alijaribu kuonesha kuwa familia yake ina furaha. Lakini mke wake Hannelore, na wanawe Walter na Petro waliathirika pia kutokana na kukosekana mara kwa mara kwa mwanasiasa huyo nyumbani.
Kiongozi wa CDU wa karne
Mwezi Juni mwaka wa 1973 Helmut Kohl alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha CDU.
Helmut Kohl ampongeza Helmut Schmidt
1982 kulikuwa na mvutano katika muungano wa uongozi wa SPD na FDP chini ya Kansela Helmut Schmidt. Kwa pamoja walimpindua Kansela Kohl. Helmut Schmidt apata ushindi na kohl anaonekana hapo akimpongeza.
Ishara nzuri ya kupatana
François Mitterrand na Helmut Kohl wanashikana mikoni. Viongozi hao walikwenda dunia nzima. Tukio: Maridhiano baina ya Ujerumani na Ufaransa katika sherehe katika makaburi ya majeshi karibu na Verdun mwaka 1984. Kohl alitaka Ujerumani iungane. Tarehe 3 Oktoba 1990 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Jamhuri ya shirikisho iliundwa.
Lawama juu Ujerumani ya mashariki
Helmut Kohl alilaumiwa kutoyashirikisha majimbo ya mashariki katika maendeleo.
Kuingia katika siasa kwa Angela Merkel
Bila ya Helmut Kohl, Kansela wa sasa Angela Merkel hangeweza kuwa kiongozi wa Ujerumani hii leo. Merkel alijifunza mengi kutoka kwa kiongozi huyo, na muungano baina ya Ujerumani ya mashariki na magharibu ndio iliomuezesha yeye kufikia wadhifa wake wa leo.
Kushindwa kwa Kohl baada ya miaka 16
KUSHINDWA KWA KOHL BAADA YA MIAKA 16 September 1998 Helmut Kohl alishindwa uchaguzi wa Ujerumani, na kumpa nafasi Gerhard Schröder Kuwa Kansela .Mwezi wa Oktoba 1998 kiongozi huyo alifanyiwa sherehe kubwa ya kuangwa.
Kashfa ya michango ya chama
Mwaka 2000, Helmut Kohl alikumbwa na kashfa kuhusu ufadhili kwa chama chake cha CDU. Kwa sababu ya ripoti ya udanganyifu iliotolewa kuhusu suala hilo , Spika wa bunge Wolfgang Thierse alikiadhibu chama hicho na kukilipisha faini ya kulipishwa Maki milioni 40 .
Kifo cha mkewe
2001 mke wa Helmut Kohl aliyeishi naye kwa miaka 41 afariki.
Mapenzi mapya
Miaka minne baada ya kifo cha mkewe ,Helmut Kohl akaowa tena mwanamke mwenye umri wa miaka 34 Maike Richter mwaka 2008.