1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maisha ya demokrasia Afrika Kusini

25 Agosti 2017

Katika vitabu anavyotunga, Sonwabiso anaangazia maisha ya vijana waliozaliwa baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Safari yao, fikra na hisia zao pamoja na matumaini ya mustakabali wao hasa wakati huu wanapoishi katika nchi yenye demokrasia

https://p.dw.com/p/2iqps

Ni miaka 21 tangu Afrika Kusini ipate demokrasia. Ili kuelezea safari hiyo, mtunga vitabu mdogo Sonwabiso Ngcowa (31) amezuru sehemu nyingi za Afrika Kusini akikusanya hadithi za watu waliozaliwa 1994. Katika kitabu chake  “21 at 21“ watu hao waliozaliwa katika enzi za demokrasia wanasimulia maisha yao, ndoto zao na matumaini yao kwa nchi.