Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amewasili Israel kuonesha mshikamano wakati huu wakipambana na Hamas, na Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel. Mchambuzi wa masuala ya diplomasia, Abbas Mwalimu Kwanza, anaeleza nafasi ya juhudi hizo na maana yake kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati.