Maharamia wa Somalia watishia kuuwa mabaharia
10 Desemba 2007NAIROBI
Maharamia wanaoshikilia meli ya mizigo ya kemikali ya Japani nje ya pwani ya mashariki kaskazini mwa Somalia wametishia kuwauwa mabaharia wa meli hiyo venginevyo wanalipwa fedha za kuwagombolea dola milioni moja.
Meli ya Golden Nori yenye kubeba maelfu kwa maelfu ya tani za kemikali ya benzene yenye kuweza kushika moto imetekwa nyara hapo tarehe 28 mwezi wa Oktoba ikiwa pamoja na mabaria wake kutoka Myanmar,Ufilipino na Korea Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa Kuratibu Masuala ya Wakimbizi OCHA maharamia hao wanataka walipwe dola milioni moja kama kigombozi wakati serikali ya Puntland imekuwa ikiwataka maharamia hao wajisalimiesha kwa amani kwenye mwambao wa Puntland.
Taarifa hiyo imesema maharamia hao wanatishia kuwauwa mababahari iwapo fedha hizo hazitolipwa.