1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Zimbabwe yatupilia mbali kesi iliyomdhalilisha rais

10 Novemba 2021

Jaji mmoja nchini Zimbabwe ameitupilia mbali kesi dhidi ya wanandoa waliosambaza picha iliyofanyiwa metengezo ya kompyuta iliyomuonyesha rais wa nchi hiyo akiwa uchi kwenye kundi la WhatsApp.

https://p.dw.com/p/42oRT
Sitz der Wahlkommision in Harare
Picha: AFP/Getty Images

Sarudzayi Ambiri Jani mwenye umri wa miaka 39 na Remember Ncube mwenye umri wa miaka 35 walikamatwa Juni 2020 kwa kusambaza picha kwenye kundi lao la majirani katika mji wa mpaka wa kusini wa Beitbridge.

Picha hiyo ilimuonyesha Rais Emmerson Mnangagwa mwenye umri wa miaka 79 akiwa uchi isipokuwa tu nembo ya chama chake cha Zanu-PF, na barakoa ikining'ing'ia kwenye uume wake.

Zimbabwe ina sheria kali ambazo zinapinga kumhujumu au kumtusi rais.

Mawakili wa wanandoa hao wamesema hakimu Takudzwa Gwazemba aliyatupilia mbali mashitaka hayo jana, akisema upande wa serikali umeshindwa kuendelea na kesi hiyo baada ya zaidi ya mwaka mmoja.