1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Zimbabwe yaamua kuwa Mnangagwa ni mshindi halali

Admin.WagnerD24 Agosti 2018

Mahakama ya katiba nchini Zimbabwe hii leo imemtihibitsha Emmerson Mnangagwa kuwa rais wa Zimbabwe na hivyo kutupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo MDC

https://p.dw.com/p/33iln
Simbabwe Harare - Nach den Wahlen: Emmerson Mnangagwa, Präsident von Simbabwe, lächelt im Anschluss an eine Pressekonferenz
Picha: picture-alliance/dpa/AP/T. Mukwazhi

Akizungumza baada ya uamuzi huo, Jaji Mkuu Luke Malaba amesema kiongozi wa upinzaniNeloson Chamisa ameshindwa kuonesha ushahidi wa namna wizi wa kura ulivyofanyika katika kipindi cha uchaguzi wa rais. Uamuzi umetolewa kwa kuzingatia uwepo wa jopo la majaji wanane.

Hali ya ulinzi na usalama imeonekana kuimarishwa mjini Harare wakati mahakama hiyo ikitoa uamuzi huo uliokuwa na majibu ya iwapo ushindi wa rais Emmerson Mnangagwa ni halali katika uchaguzi wa kwanza wa kihistoria nchini humo. Upinzani ulidai kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo na kutaka uchaguzi mpya au kutangazwa mgombea wake Nelson Chamisa mshindi wa uchaguzi huo. Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ilimtangaza Mngagwa kushinda  kwa asilimia 50.8 huku Chamisa akipata asilimia 44.3.

Kumbukumbu ya uchaguzi

Simbabwe Wahlen Nelson Chamisa
Kiongozi wa harakati za upinzani Zimbabwe MDC Nelson ChamisaPicha: Reuters/P. Bulawayo

Kimsingi uchaguzi huo, uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya Mnangagwa na kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa ambao pia ulikuwa wa mchuano mkali, ulitazamwa kama hatua muhimu katika kuelekea kuufufua uchumi na kuondosha taswira mbaya ya zimbabwe lakini badala yake umelifanya taifa hilo kuzorota kabisa. Ukandamizaji uliofanywa na jeshi mwezi Agosti, kufuatia vurugu za baada ya uchaguzi ulisababisha watu 6 kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa katiba ya Zimbabwe baada ya kutangazwa mshindi Mnangagwa atapaswa kuapishwa Jumapili ijayo. Awali mwanasheria wa mpinzani Chamisa, aliituhumu Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ZEC kuongeza kiasi cha kura 69,000 kwa lengo la kuepusha uchaguzi wa marudio. Na kwamba matokeo ya ZEC yalikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba udanganyifu umefanyika.

Wachambuzi wanasema kuwa Mnangagwa sasa atakabiliwa na changamoto na lawama za jumuiya ya kimatiafa kuhusiana na ukandamizaji wa jeshi dhidi ya umma wa wananchi, pamoja na changamoto nyingine za mabadiliko ya kiuchumi ili kuweza kulifanya taifa Zimbabwe lisonge mbele.

Vizuizi vya polisi vimewekwa katika eneo la mahakama, jengo karne ya 19 na kutumia wa ukoloni, likiwa mkabala na ofisi ya Mnangagwa mjini Harare. Magari ya ya maji ya kuwasaha yamekuwa yakizunguka katika eneo la jengo la mahakama huku polisi wa kutuliza ghasia kwa makundi kwa makundi wakipiga doria katika eneo la katikati ya jiji.

Ushindi wa mnangagwa ulitabiriwa mapema sana, kwa mfano gazeti linalomiliwa na serikali la Herald limeandika "Uamizi ukishatolewa amani lazima ilindwe." Huku gazeti lingine la kibinafsi Zimbabwe Independet likisema uamuzi wa mahakama hauwezi kuegemea upande wa Chamisa.

Pamoja na yote hayo idadi kubwa ya Wazimbabwe, walikwenda katika majukumu yao ya kawaida. Zimambwe kwa wakati huu ipo katika ukata wa uwekezaji wa kigeni, ikiwa sehemu ya tatizo la mgogoro wa kiuchumi kwa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR

Mhariri:Iddi Ssessanga