1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaamua Klasnic alipwe fidia

31 Machi 2017

Aliyekuwa kocha wa Croatia na Werder Bremen Ivan Klasnic ataüokea euro 100,000 kama fidia kutoka kwa madaktari wawili ambao mahakama imewakuta na hatia ya kutotambua vizuri matatizo yake ya figo

https://p.dw.com/p/2aQAb
Kroatien Ivan Klasnic Milchbauer
Picha: SBplus/Aleksandra Primorac

Mahakama ya Bremen pia imeamuru kuwa madaktari hao wawili lazima walipe gharama zote za matibabu ya zamani na ya usoni na kuwa Klasnic anaweza kudai fidia kwa kupoteza mapato yake.

Mahakama imesema daktari wa zamani wa timu ya Bremen Goetz Dimanski na mtalaamu wa  daa za ndani ya mwili Manju Guha walipaswa kugundua matatizo ya figo ya Klasnic na kuyatibu kabla ya kufichuliwa wakati  wa operesheni ya mwaka wa 2005. Klasnic ambaye sasa ana umri wa miaka 37, alifanyiwa upandikiziaji mara mbili mwaka wa 2007 lakini sasa anahitaji upandikiziaji mwingine kwa sababu kiungo alichopewa kutoka kwa babake hakifanyi kazi vizuri.

Anahitaji kusaifiwa damu mara kwa mara. Aliichezea Bremen 2001-2008 ambapo alishinda mataji mawili msimu wa 2004: la Bundesliga na kombe la shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB Pokal. Pia aliichezea Mainz, Bolton na Nantes, na akaichezea Croatia mechi 41 kati ya 2004 na 2011.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman