1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Ujerumani yaifungulia njia Euro

12 Septemba 2012

Mahakama Kuu ya Katiba imefungua njia ya kuidhinishwa mpango wa kudhamini utulivu wa sarafu ya Euro na kuondowa hofu zilizokuwepo kuhusu namna ya kushughulikiwa mgogoro wa madeni miongoni mwa nchi za kanda ya Euro.

https://p.dw.com/p/167DX
Mahakimu wa korti kuu ya katibaPicha: Reuters

Mahakimu wa mjini Karlsruhe wameyakataa kwa sehemu kubwa madai kwamba rais wa shirikisho asiachiwe kuidhinisha mpango huo hadi hukmu ya mwisho itakapotolewa kama mpango huo unaambatana au la na katiba ya Ujerumani.

Kwa kupitisha uamuzi huo uliokuwa ukisuburiwa kwa hamu kubwa,mahakimu wakuu wanane wamempa ruhusa rais wa shirikisho Joachim Gauck aidhinishe nyaraka kuhusu mustakbal wa mpango wa kudhamini utulivu wa sarafu ya Euro-ESM na mpango wa kuleta utulivu wa bajeti iliyoidhinishwa na bunge mwishoni mwa mwezi June lakini ikakwama kutokana na malalamiko kadhaa yaliyotolewa dhidi ya mipango hiyo.

Mahakimu wakuu wa korti ya katiba mjini Karlsruhe wameyakataa pia madai dhidi ya mpango uliotangazwa na benki kuu ya Ulaya wa kununua dhamana za mikopo katika nchi zinazokabwa na migogoro ya kiuchumi.

Uamuzi wa korti kuu ya katiba umefungamanishwa lakini na masharti yanayotaka bunge la shirikisho Bundestag litoe idhini yake ikiwa Ujerumani italazimika kulipiaa kiwango chocchote chote kitakapopindukia Euro bilioni 190.

Spika wa bunge la katiba Andreas Voßkuhle anasema:

"Kwa niaba ya umma,madai ya kuamuru uzuwiliwe mkataba wa kuanzishwa mpango wa kudhamini utulivu wa sarafu ya Euro yamekataliwa.Mpango huo lakini utaweza kuidhinishwa tu ikiwa kifungu nambari nane,kiungo cha 5,mstari wa kwanza ,kinachohusiana na kiwango cha juu cha fedha ,kitapata ridhaa ya mabaraza yote mawili bunge la shirikisho Bundestag na baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat."

Symbolbild Bundesverfassungsgericht Euro-Rettungsschirm ESM
Kitambulisho cha uamuzi wa korti kuu ya katiba kuhusu mpango wa kudhamaini utulivu wa sarafu ya EuroPicha: picture-alliance/dpa

Kinyume na mashtaka sita yaliyotumwa na wabunge,na hasa wale wa chama cha mrengo wa shoto-Die Linke,mahakimu wakuu wa korti ya katiba wanasema mpango wa kudhamini utulivu wa sarafu ya Euro unaambatana na kwa sehemu kubwa na muongozo wa katiba unaotaja kwamba suala la bajeti ni suala linalobidi kushughulikiwa na bunge la shirikisho tu-Bundestag.

Bundesverfassungsgericht Urteil zum ESM Reaktionen an der Börse
Soko la hisa la Frankfurt baada ya uamuzi wa mahakimu wa KarlsruhePicha: Reuters

Soko la hisa la mjini Frankfurt limepokea vyema uamuzi wa mahakimu wa korti ya katiba.Faharasa za soko la Dax zimeongezeka kwa asili mia 1.08 na kufikia pointi 7.388.98 huku soko la Mdax likifuata mkondo huo huo na kujikingia pointi 11.262.99

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/afp

Mhariri:Mohamed Khelef