1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUfilipino

Mahakama ya Ufilipino yamkuta bila hatia Maria Ressa

12 Septemba 2023

Mahakama nchini Ufilipino imemkuta bila hatia mwanahabari na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Ressa, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kukwepa kulipa kodi.

https://p.dw.com/p/4WDh7
Philippinen Rodrigo Duterte
Aliekuwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte 2018-2022Picha: Bullit Marquez/AP Photo/picture alliance

Maria Ressa, mwenye umri wa miaka 59, alikabiliwa na msururu wa mashitaka wakati wa utawala wa rais wa zamani Rodrigo Duterte aliyeitawala Ufilipino kuanzia mwaka 2016 hadi 2022, baada ya kuwa mkosoaji mkubwa wa sera ya kikatili ya Duterte ya kukabiliana na madawa ya kulevya.

Soma pia:Ufilipino na Australia zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati

Mwezi Januari, Mahakama ilimfutia mashtaka manne ya kwanza.

Licha ya ushindi huu wa kisheria, mustakabali wa Bi Ressa bado haujulikani kwani bado anakabiliwa na kesi nyingine mbili.