Mahakama ya Rwanda yamkuta Rusesabagina na hatia ya ugaidi
20 Septemba 2021Waendesha mashtaka wa Rwanda wametaka Rusesabagina, shujaa ambaye simulizi yake ilihamasisha filamu iliyopewa jina ''Hotel Rwanda'' ahukumiwe kifungo cha maisha jela.
Soma pia: 'Shujaa wa Hotel Rwanda' kukabiliwa na miaka 25 jela
Rusesabagina ambaye alitumia umaarufu wake kumkosoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kama dikteta, alikamatwa Agosti mwaka 2020 mjini Kigali.
Soma pia: Mpinzani wa kisiasa akamatwa kwa madai ya ubakaji Rwanda
Rusesabagina, mwenye umri wa miaka 67 aliyesaidia kuwaokoa maelfu ya watu katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, alishtakiwa kwa makosa tisa ikiwemo kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi, kufadhili ugaidi, mauaji na ujambazi wa kutumia silaha.
Soma pia: Kesi ya ugaidi dhidi ya Rusesabagina yaanza mjini Kigali
Mashtaka hayo yanahusiana na mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la National Liberation Front FLN nchini Rwanda kati ya mwaka 2018 na 2019.