1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaruhusu utekelezaji wa sheria ya fedha, 2023

28 Julai 2023

Mahakama Kuu nchini Kenya leo imeondowa amri ya kusitishwa utekelezwaji wa nyongeza ya ushuru mpya uliozua utata.

https://p.dw.com/p/4UWId
Kenias Präsident William Ruto
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Hatua hiyo pia ilisababisha maandamano ya upinzani hadi uamuzi wa kesi ya rufaa utakapotolewa.

Mswada wa fedha wa mwaka 2023 ulikuwa umefungua njia kwa serikali kuongeza ushuru kuanzia Julai 1.

Mahakama hiyo imechukua uamuzi huo baada ya seneta wa kaunti ya Busia Okiya Omutata kuwasilisha kesi mahakamani kupinga uhalali wake wa kikatiba.

Rais William Ruto mwezi uliopita alitia saini na kuwa sheria mswada wa fedha uliotarajiwa kuiingiza serikali kipato cha zaidi ya dola bilioni 2.1, japo nyongeza hiyo ya ushuru ilitishia kuongeza mzigo kwa wananchi ambao tayari walikuwa wanakabiliwa na mfumuko wa bei. 

Uamuzi huo unatokea licha ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali kulalamikia gharama ya juu ya maisha, huku maandamano hayo yakigeuka ya vurugu.