1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya rufaa Kenya kuamua kuhusu mageuzi ya katiba

20 Agosti 2021

Uamuzi kuhusu mchakato wa kuibadilisha katiba ya Kenya kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa maarufu kama BBI unaosubiriwa kwa hamu kutolewa leo Ijumaa.

https://p.dw.com/p/3zE5x
Kenia Nairobi - Oberster Gerichtshof
Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

Mahakama ya rufaa ya Kenya itatoa hukumu leo kuhusu ombi la rais Uhuru Kenyatta kuibadili katiba katika uamuzi ambao huenda ukabadili kabisa ulingo wa siasa huku nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani.

Rais Kenyatta anahoji mapendekezo yake ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2010 yatasaidia kuepusha machafuko ya kila baada ya uchaguzi, suala tete ambalo limewagawa viongozi wa kisiasa nchini humo.

Mapendekezo hayo yaliridhiwa na bunge mnamo mwezi Mei mwaka huu na yalitarajiwa kupigiwa kura ya maoni, lakini siku mbili baadaye, mahakama kuu ya mjini Nairobi ikapitisha hukumu ikisema mapendekezo hayo hayakuwa halali kwa kuwa rais hana mamlaka ya kuanzisha mchakato huo.