Vikwazo Venezuela ilivyowekewa na EU vyatupiliwa mbali
13 Septemba 2023Matangazo
Majaji wamepitisha uamuzi kwamba hatua za kuiadhibu Venezuela zilizochukuliwa na Umoja wa Ulaya zilikuwa na msingi kutokana na kushuhudiwa, vurugu,matumizi makubwa ya nguvu,ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na kitisho kwa demokrasia nchini humo.
Kwa mujibu wa majaji,kulikuwa na ushahidi wa kutosha wakati Umoja wa Ulaya ulipopitisha vikwazo dhidi ya Venezuela mwaka 2017.
Nchi hiyo imetowa hoja kwamba vikwazo vya Umoja wa Ulaya vimetokana na makosa ya kutengenezwa wakati hali ya kisiasa ya nchi hiyo ikipothminiwa.
Venezuela hata hivyo inaweza kuupinga uamuzi wa mahakama ya Luxenmbourg katika mahakama ya juu kabisa ya haki ya Umoja wa Ulaya, ECJ.