Mahakama ya Lebanon yaamuru wanajeshi wakamatwe
3 Februari 2008Mahakama moja nchini Lebanon imeamuru maafisa watatu wa jeshi na wanajeshi wanane wakamatwe kuhusiana na mauaji ya waandamanaji wa upinzani yaliyofanywa wiki moja iliyopita katika mojawapo ya machafuko ya umwagaji damu kuwahi kutokea tangu vita vya kikabilia vya kati ya mwaka wa 1975 na 1990.
Jaji wa mahakama hiyo ameamuru raia sita wakamatwe kwa kuandamana na kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Wanajeshi wa Lebanon walifyatua risasi kuyavunja maandamano ya upinzani ya kupinga mgao wa umeme katika kitongoji cha mjini Beirut Jumapili wiki iliyopita.
Wafuasi saba waliuwawa na wengine 30 kujeruhiwa katika tukio hilo.
Kundi la Hezbollah limesema jeshi la Lebanon halikuyashughuhulikia vizuri maandamano hayo na limetaka uchunguzi ufanywe haraka.