1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu yatupilia mbali ombi la Kenya

31 Agosti 2011

Jana mahakama ya kimataifa ya uhalifu ilitupilia mbali rufani iliowasilishwa na serikali ya Kenya kutaka kesi ya maafisa wake sita wakuu waliohusika katika machafuko baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 isikilizwe Kenya.

https://p.dw.com/p/12QLg
Mahakama ya Uhalifu mjini The Hague, UholanziPicha: picture-alliance/ANP XTRA

Baadhi ya wale wanaotuhumiwa mbele ya mahakama hiyo, kama vile waziri wa zamani wa elimu ya juu, William Ruto, waziri wa zamani wa viwanda, Henry Kosgey, na afisa mkuu wa redio, Joshua Arap Sang, wameshawasili the Hague kwa ajili ya kesi hiyo hapo kesho.

Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na waziri wa utalii wa Kenya, Najib Balala, aliyekuweko Mombasa, na alimuomba ampe tathmini yake juu ya uamuzi wa jana wa mahakama ya The Hague, na athari ya kesi kwa siasa za ndani za Kenya.

Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Mohamed Abdulrahman