1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Katiba ya Croatia yamzuwia rais kuwa waziri mkuu

19 Aprili 2024

Mahakama ya Katiba nchini Croatia imepitisha uamuzi wa kumzuia Rais Zoran Milanovic kuchukuwa nafasi ya waziri mkuu yenye madaraka makubwa zaidi baada ya uchaguzi uliofanyika wiki hii.

https://p.dw.com/p/4ezUR
Rais Zoran Milanovic wa Croatia
Rais Zoran Milanovic wa CroatiaPicha: Antonio Bronic/REUTERS

Hatua hiyo inazima azma ya kiongozi huyo ya kutaka kuongoza serikali yoyote ya muungano nchini humo.

Mahakama hiyo ilisema siku ya Ijumaa (Aprili 19) kwamba Rais Milanovic alishindwa kuzingatia onyo lililotolewa mnamo mwezi Marchi la kumtaka kwanza ajiuzulu nafasi ya urais  kabla ya kuanza kampeni ya kutaka wadhifa wa uwaziri mkuu.

Soma zaidi: EU yapongeza mafanikio makubwa ya Croatia

Kiongozi huyo wa Croatia mara kadhaa ameukosoa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na amekuwa akipinga hatua ya kuisadia Ukraine katika vita vyake na Urusi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW