1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mchakato wa kusikiza hoja kuhusu wahamiaji kuanza Uingereza

9 Oktoba 2023

Mahakama ya Juu ya Uingereza inaanza leo mchakato wa siku tatu kusikiliza hoja juu ya uhalali wa nchi hiyo kupeleka nchini Rwanda, wahamiaji wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria

https://p.dw.com/p/4XH4P
Wahamiaji wakusanyaika mjini Casablanca nchini Morocco mnamo Januari 19, 2023
Wahamiaji mjini Casablanca nchini MoroccoPicha: Fadel Senna/AFP/Getty Images

Mchakato huo unaanza baada ya serikali ya chama cha Conservative kukataa rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa wa mwezi Juni, ambao ulisema mpango huo wa serikali ni kinyume cha sheria, kwa sababu Rwanda sio nchi salama.

Marekani na nchi za Ulaya zapambana na mawimbi ya wahamiaji

Haya yanajiri wakati Marekani na nchi nyingi za Ulaya zikipambana kutafuta njia bora ya kukabiliana na mawimbi ya wahamiaji wanaoingia katika nchi hizo kutafuta hifadhi, wakikimbia vita, ghasia na ukandamizaji, pamoja na madhila yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Soma pia: Brussels yakosa muafaka mgogoro wa wakimbizi

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anaupigia upatu mpango huo wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda kama suluhisho mwafaka, lakini unapingwa vikali na watetezi wa haki za binadamu pamoja na watu wengi maarufu nchini Uingereza.