1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya juu Michigan yakataa jaribio la kumuondoa Trump

27 Desemba 2023

Mahakama ya juu katika jimbo la Michigan Marekani, imekataa jaribio la kumuondoa rais wa zamani wa taifa hilo Donald Trump katika uchaguzi wa mwaka 2024.

https://p.dw.com/p/4ad7l
New York City | Aliekuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Aliekuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Louis Lanzano/UPI Photo/IMAGO

Hatua hiyo ni chini ya kifungu cha katiba cha marufuku ya uasi, kinachowapiga marufuku wanasiasa wanaotuhumiwa kuiasi katiba kushika wadhifa wa Urais. 

Umauzi huo unakinzana na ule uliotolewa wiki iliyopita na mahakama ya  Colorado iliyosema Trump hana sifa ya kushikia wadhifa wa rais na kumpiga marufuku pia ya kushiriki uchaguzi wa kuwateua wagombea wa urais katika jimbo la Colordo. 

Soma pia: Mahakama Colorado imemzuia Donald Trump kuwania urais jimboni humo

Uamuzi huo ulitolewa kufuatia jukumu lake katika uvamizi wa Januari 6, 2021 uliofanywa na wafuasi wake kwenye makao makuu ya bunge la Marekani mjini Washington.