1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya juu yasema Trump ana kinga ya kutoshitakiwa

2 Julai 2024

Mahakama ya juu nchini Marekani jana ilitoa uamuzi kwamba Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump hawezi kufunguliwa mashtaka kwa vitendo ambavyo vilikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba wakati akiwa rais.

https://p.dw.com/p/4hl1Y
USA New York 2024 | Ehemaliger Präsident Donald Trump bei Gerichtsprozess
Picha: Mike Segar/REUTERS

Mahakama ya juu nchini Marekani jana ilitoa uamuzi kwamba Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump hawezi kufunguliwa mashtaka kwa vitendo ambavyo vilikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba wakati akiwa rais.

Trump apatikana na hatia katika kesi ya uhalifu

Uamuzi huo huenda ukachelewesha kesi yake ya kula njama ya kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020. Uamuzi huo wa majaji wa mahakama ya juu waliogawika, umetolewa miezi minne kabla ya uchaguzi wa rais ambapo Trump atakabiliana na Joe Biden.

Jaji Mkuu Mhafidhina John Roberts, alisema kuwa rais "hayuko juu ya sheria" lakini ana "kinga kamili" dhidi ya kufunguliwa mashitaka ya jinai kwa matendo yanayofanyika pindi akiwa madarakani.

Majaji ambao hawakukubaliana na uamuzi huo, wamekosoa vikali na kuibua wasiwasi juu ya mustakabali wa kidemokrasia wa nchi hiyo. Trump ameutaja uamuzi huo kuwa ni "ushindi mkubwa."