1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya ICC yaionya Jubilee, Kenya

Josephat Nyiro Charo4 Septemba 2013

Onyo hilo linakuja huku bunge la Kenya likitarajiwa kukutana Alhamisi (05.09.2013) kujadili kesi zinazowakabili viongozi wa muungano wa Jubilee katika mahakama ya mjini The Hague.

https://p.dw.com/p/19bZm
Kenya's Deputy Prime Minister Uhuru Kenyatta (R), who is also the Jubilee Alliance Presidential candidate, speaks with his running mate William Ruto on February 13 ,2013 before addresses supporters during a political rally in the capital Nairobi, ahead of next month's general election. AFP PHOTO/ SIMON MAINA (Photo credit should read SIMON MAINA/AFP/Getty Images)
Kenia Wahlen Uhuru Kenyatta und William RutoPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu, ICC, ya mjini The Hague Uholanzi imeuonya muungano wa Jubilee kwa nia yake ya kutaka kuiondoa Kenya kutoka kwa mkataba wa Roma ulioiunda mahakama hiyo. Mahakama hiyo imesema hatua hiyo haitasaidia kuzikwamisha kesi zinazowakabili viongozi wa muungano huo. Kesi dhidi ya Makamu wa rais, William Ruto, pamoja na mwanahabari Joshua Arap Sang, inatarajiwa kuanza katika mahakama hiyo Septemba 10 huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kwenda Hague Novemba 12 mwaka huu kwa ajili ya kujibu mashitaka kuhusiana na machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Sikiliza mahojiano kati ya Josephat Charo na mwanaharakati wa haki za binaadamu na haki za kiraia nchini Kenya, Gachihi Gacheke, ambaye kwanza anatoa maoni yake kuhusu mambo yanavyokwenda katika kesi za viongozi hao wa Jubilee. Kusikiliza mahojiano haya tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Yusuf Saumu