1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni kinyume cha sheria kwa Ujerumani kubadili fedha za bajeti

15 Novemba 2023

Mahakama ya juu nchini Ujerumani imesema hatua ya serikali ya kubadilisha matumizi ya fedha katika bajeti inakiuka katiba.

https://p.dw.com/p/4YqYt
Deutschland|Kansela Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Marijan Murat/dpa/picture alliance

Mahakama hiyo ya juu katika mji wa Karlsruhe imeeleza kwamba serikali ya Ujerumani haiwezi kutumia fedha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ambazo zilitengwa kwa ajili ya kupambana na janga la corona. 


Jaji wa mahakama hiyo Doris König wakati wa kutoa uamuzi huo amesema ni swala la kuzingatia ukomo wa kukopa. Uamuzi huo umewapa ushindi kambi ya Upinzani ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU ambavyo vilipinga hatua ya serikali ya kubadilisha matumizi ya fedha yaliyopitishwa kwenye bajeti.

Serikali ya Ujerumani yadaiwa kukiuka katiba katika kazi zake

Kutokana na janga la Covid-19 mnamo ya mwaka 2021 serikali ya Ujerumani iliongeza bajeti ya dharura kwa Euro bilioni 60 kwa njia ya mikopo.
Katika hali za dharura kama hizo serikali inaweza kuvuka kiwango kinachoruhusiwa kukopa.

Baada ya uamuzi huo wa mahakama ya juu, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema uamuzi huo unaweza kuwa na athari katika mipango ya bajeti. Scholz amelieleza Bunge kwamba serikali inapasa kutafuta njia nyingine za kutafuta fedha kwa ajili ya uwekezaji.