Mahakama Ujerumani yahalalisha wanahabari kufuatiliwa
29 Novemba 2023Mahakama moja ya kusini mwa Ujerumani imetoa uamuzi kuwa kundi la wanaharakati wa mazingira la Kizazi cha Mwisho ni tishio kubwa kwa usalama wa raia na hiyo inahalalisha kufuatilia mawasiliano ya simu kati ya waandishi habari na maafisa wa mawasiliano wa kundi hilo.
Mahakama ya wilaya mjini Munich imekataa malalamiko kadhaa yaliyowasilishwa na waandishi habari kuhusiana na ufuatiliaji wa polisi wa mawasiliano yao na kundi hilo la wanaharakati, linalofahamika sana Ujerumani kwa kuyazuia magari barabarani.
Soma pia:Polisi Kenya yazuia mkutano wa wanaharakati na wanahabari
Maafisa jimboni Bavaria kwa miezi kadhaa wamekuwa wakiwachunguza wanachama wa kundi hilo kwa tuhuma za kuunda shirika la uhalifu, na wamefanya misako kadhaa ya makaazi yao na upekuzi mwingine.
Mahakama imesema kuwa kitisho kinachowekwa na wanaharakati hao kinahalalisha ukiukaji wa uhuru wa vyombo vya habari.