1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Uhispania kuamua kuhusu mgomo wa wachezaji

12 Mei 2015

Mahakama nchini Uhispania itaamua Jumatano juu ya uhalali wa mgomo wa kupinga sheria mpya ya haki za kutangaza michezo ya kandanda katika televisheni uliotishwa na chama cha wachezaji kandanda

https://p.dw.com/p/1FOeh
Real Madrid-Stadion Santiago Bernabeu
Picha: Getty Images

Chama hicho kinatishia kuchafua michezo miwili ya mwisho katika La Liga na pia fainali ya kombe la mfalme. Chama hicho kimetangaza wiki iliyopita kwamba wachezaji watagoma kuingia viwanjani kuanzia Mei 16, na ligi ya wachezaji wa kulipwa LFP, ambayo inawakilisha vilabu 42 katika madaraja ya juu , imepeleka pingamizi kwa hatua hiyo kutangazwa kuwa si halali.

Nchini Italia, AS Roma imeendelea kushika nafasi ya pili na kujipatia nafasi ya kucheza katika Champions League , licha ya kuteleza kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya AC Milan. Napoli iko pointi tatu nyuma ya Lazio baada ya kutoka sare ya mabo 2-2 dhidi ya Parma. Cesena inajiunga na Parma kuelekea Serie A msimu ujao baada ya kugaragazwa na sassuolo kwa mabao 3-2.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae / ape / afpe
Mhariri: Iddi Ssessanga