MigogoroRwanda
Korti Rwanda yamhukumu miaka 20 mtuhumiwa mauaji ya kimbari
6 Septemba 2024Matangazo
Venant Rutunga mwenye miaka 75, alirudishwa Rwanda kutokea Uholanzi mwaka 2021 alikofunguliwa mashitaka kuhusiana na madai kwamba aliagiza kufanyika mauaji hayo zaidi ya robo karne iliyopita.
Soma pia: Wiki ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda
Kulingana na mwendesha mashitaka, Rutunga aliwapeleka polisi kwenye taasisi ya utafiti wa kilimo kulikokuwa na wafanyakazi wa Kitutsi na watu wengine waliokuwa wamejificha, ambao wote waliuawa. Rutunga aliwahi kuwa mkurugenzi wa kikanda wa taasisi hiyo ya ISAR.
Rutunga, aliyekana mashtaka, alidai kuwa aliwaita maafisa hao ili kulinda usalama, uamuzi ambao alisema uliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya ISAR.