SiasaPakistan
Mahakama Pakistan yatoa uamuzi kuhusu uchaguzi wa mikoa
4 Aprili 2023Matangazo
Wakili Ali Zafar, wa chama cha Imran Khan, Tahreek-e-Insaf, amesema jopo la majaji watatu linaloongozwa na jaji mkuu Umar Ata Bandyal limeitaja Mei 14 kama terehe mpya ya uchaguzi.
Mnamo Machi 22 bodi ya uchaguzi iliahirisha uchaguzi katika jimbo la Punjab hadi Oktoba 8 kutokana na ukosefu wa fedha na usalama. Tarehe ya kufanyika uchaguzi jimbo la Khyber Pakhtunkhwa ilikuwa ikidurusiwa upya wakati jopo liliposema uchaguzi katika jimbo hilo haungeweza kufanyika kutokana na terehe ya mwisho kikatiba.
Zafar amesema mahakama imeitaka serikali itoe fedha kwa bodi ya uchaguzi na imewataka maafisa wote wa serikali za mikoa na shirikisho wasaidie kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa amani.