1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Nigeria kuamua kuhusu ushindi wa Tinubu

6 Septemba 2023

Mahakama ya uchaguzi nchini Nigeria hii leo itatoa uamuzi kuhusu uhalali wa ushindi wa rais Bola Tinubu baada ya madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4W0CN
Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Gbemiga Olamikan/AP/dpa/picture alliance

Mahakama ya uchaguzi nchini Nigeria hii leo itatoa uamuzi kuhusu uhalali wa ushindi wa rais Bola Tinubu baada ya madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi.

Aliyekuwa mgombea wa urais Atiku Abubakar wa chama cha People's Democratic na Peter Obi wa chama cha Labour waliwasilisha madai ya ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kushindwa kutumia mashine za kielektroniki kunakili matokeo ya vituo vya kupigia kura.

Tume ya uchaguzi nchini humo INEC ilikiri kuwepo kwa makosa ingawa ilikana madai kwamba uchaguzi huo ulihujumiwa.

Katika uchaguzi huo wa mwezi Februaria uliokumbwa na mivutano, gavana wa zamani wa Lagos Bola Tinubu alishinda kwa asilimia 37.

Vyama hivyo vyote viliwasilisha mapingamizi tofauti ya kushinikiza matokeo hayo kubatilishwa na wagombea wao kutangazwa washindi ama kupelekwa mahakamani ili uchaguzi huo urudiwe.