SiasaYemen
Mahakama moja Yemen yawahukumu kifungo wanaharakati wanne
21 Machi 2023Matangazo
Wanaharakati hao wanatuhumiwa kuwakosoa kupitia mitandao ya kijamii, waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.
Kwa mujibu wa wakili wao Waddah Qutaish wanaharakati hao walishtakiwa kwa kuchochea vurugu,kuvuruga amani pamoja na kutumia lugha chafu dhidi ya waasi wa kihouthi.
Soma pia:Pande zinazohasimiana Yemen kubadilishana wafungwa
Walikamatwa na kuzuiliwa mjini Sanaa mwezi Desemba na Januari kwa mashataka yaliyotokana na vidio walizochapisha katika mitandao ya kijamii mwaka jana,wakiwakosoa wahouthi kufuatia madai ya kuhusishwa na rushwa na namna wanavyoshughulikia uchumi.