Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha iliyopo kaskazini mwa Tanzania kuwaachia huru wananchi 24 wa Loliondo waliokuwa wanatuhumiwa kwa mauaji ya afisa mmoja wa jeshi la polisi, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa wanasiasa wakitaka serikali ya nchi hiyo kurekebisha mfumo wa upelelezi wa makosa wa jinai. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Veronica Natalis.