Mwendesha mashitaka Kenya ameagiza viongozi wa muunganao wa upinzani NASA, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, wahojiwe kuhusiana na kauli zao walizotoa kuwa uchaguzi mpya wa Oktoba 26 hautafanyika.
Mahakama ya Juu iliamuru uchaguzi mkuu urudiwe baada ya kufuta matokeo ya awali ya uchaguzi wa August 8, ambapo rais Uhuru Kenyatta alishinda. DW imezungumza na mmoja wa wachambuzi nchini humo, Herman Manyora ambaye anatoa maoni yake kuhusiana na hatua hiyo.