1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuatemala

Mahakama Guatemala yaamuru duru mpya ya uchaguzi

13 Julai 2023

Mahakama Kuu ya Uchaguzi nchini Guatemala imeruhusu kufanyike duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwezi ujao na hivyo kuhitimisha mvutano wa kisheria baada ya duru ya kwanza iliyofanyika Juni 25 kugubikwa na hitilafu.

https://p.dw.com/p/4Todp
Guatemala I Wahlergebnisse der ersten Runde  werden bestätigt
Picha: Orlando Estrada/AFP/Getty Images

Wagombea wawili katika kinyang'anyiro hicho ni Sandra Torres na Bernardo Arevalo wanaotetea sera za kijamii na kidemokrasia na ambao wanatarajia kuiongoza nchi hiyo ya Amerika ya Kati inayokumbwa na umaskini, rushwa na ghasia za magenge.

Iwe Torres au Arevalo atakaeibuka mshindi, hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha muongo mmoja, nchi hiyo kutawaliwa na rais wa mrengo wa kushoto.

Torres ni mke wa rais wa zamani Alvaro Colom na Arevalo ni mtoto wa rais wa zamani Juan Jose Arevalo.