Kardinali Pell ashindwa rufaa ya hatia ya ngono kwa watoto
21 Agosti 2019Pell ataendelea kutumikia kifungo chake cha miaka sita kwa kuwashambulia kingono wavulana wawili wenye umri wa miaka 13 waliokuwa wanaimba kwaya kwenye kanisa mjini Melbourne katika miaka ya 1990.
Pell mwenye umri wa miaka 78 alikuwa amevaa suti nyeusi na mara kwa mara alikuwa akiinamisha kichwa chake wakati Jaji Mkuu Anne Ferguson akisoma hukmu yake huku kundi la watu lililokusanyika nje ya mahakama hiyo likishangilia.
Jaji Ferguson alisema Pell atakuwa atastahili kupewa msamaha baada ya miaka mitatu na miezi minane, ingawa Kardinali huyo anaweza bado kuiomba mahakama ya juu ya Australi kusikiliza rufaa zaidi.
Pell ndiye kiongozi wa juu zaidi wa Kikatoliki kutiwa hatiani kwa makosa ya udhalilishaji wa watoto kingono, na kuifanya kesi yake pamoja na hukumu ya leo wakati wa uthibitisho kwa waumini na makundi ya wahanga kote duniani.
Alisaidia huko nyuma kuwachagua mapapa, alisimamia hazina ya Vatican na alishiriki katika uitikiaji wa Kanisa la Australia juu ya madai ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto.
Hukumu yawapa imani wahanga
Pam Stavropoulos, kutoka kundi la watoto walioathirika, amesema kwa manusura wengi, kuthibitishwa kwa hatia dhidi ya mkosaji mashuhuri na aliewahi kuwa na mamlaka makubwa, kunatilia mkazo imani katika mchakato wa kisheria na uwezekano wa kuzungumza waziwazi.
Mawakili wa Pell waliainisha vipingamizi 13 dhidi ya hatia zake, na kutilia mashaka kila kitu kuanzia uwezekano wa kimwili wa Pell kuvua majojo yake kumbaka mvulana, hadi kwenye uaminifu wa shahidi mkuu. Kesi hiyo haikuwa ya kawaida kwa sababu ilitegemea zaidi ushahidi wa mhanga pekee aliesalia hai.
Wawili kati ya majaji wamemuelezea mhanga kama shahidi mwenye "heshima" ambaye hakuwa muongo, asie na njozi na shahidi wa ukweli." Mmoja wa wahanga wa Pell alitoa maoni yake katika taarifa iliyosomwa na wakili wake Vivian Waller, baada ya hukumu ya mahakama dhidi ya rufaa ya Pell.
"Nimetulizwa na uamuzi wa mahakama ya rufaa. Ni miaka minne sasa tangu niliporipoti polisi. Mchakato wa jinai umekuwa wa kuchokesha. Safari hiyo imenipeleka maeneo mengi, ambayo nilihofia kwamba nisingeweza kurejea. Lakini nashukuru kwamba mahakama imempa Pell fursa ya kupinga mashtaka, na kila fursa ya kusikilizwa. Natumai tu kwamba sasa yote yameisha."
Wakili wa mtoto wa baba ya mtoto wa pili --- ambaye alifariki kutokana na kubugia madawa madawa 2014 --- amesema alihisi kuondolewa mzigo mzito mabegani kwake. Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison ameelezea huruma kwa wahanga hao, na kusema mahakama imefanya kazi yake, na amesema Kardinali Pell atanyang'anywa nishati yake ya heshima baada ya kushindwa rufaa yake.
Chanzo: Mashirika