Katiba zinazuwia Tume za Uchaguzi kushitakiwa mahakamani
Mohammed Khelef16 Februari 2016
Licha ya Rais John Pombe Magufuli kujivua kwenye utatuzi wa mkwamo wa kisiasa unaovikumba visiwa vya Zanzibar akidai kuwa hana mamlaka ya kuingilia uhuru wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC), wanasheria wanasema ushauri wake wa kuwataka wasiokubaliana na uamuzi wa ZEC kwenda mahakamani unakwenda kinyume na uhalisia.