Mageuzi makubwa kufanywa katika jeshi la Ujerumani
24 Agosti 2010Matangazo
Waziri Guttenberg amesema, anataka kupunguza idadi ya wanajeshi kwa theluthi moja yaani kutoka 250,000 hadi kama 163,000. Vile vile amependekeza kuondoa utaratibu wa kuandikisha wanajeshi kwa mujibu wa sheria, lakini amesema, sheria hiyo isiondoshwe bali iendelee kubakia katika katiba ya nchi. Kwa kufanya mageuzi hayo, jeshi litapunguza gharama zake na litakuwa na vikosi vilivyoandaliwa bora zaidi kwa operesheni zake na bila ya kuhatarisha usalama wa ndani alieleza waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg.
Mwandishi: P.Martin/ZPR