Magazetini:Kampeni zapamba moto uchaguzi wa Ujerumani
12 Septemba 2017Tukianza na gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe, linazungumzia kuhusu kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika hapo Septemba 24. Mhariri anaandika:
Katika mapambano ya vyama kuwania kushika nafasi ya tatu hili ni suala, linalohusu idadi ya viti na heshima, nani atakuwa juu ya vyama vingine vidogo. Kwa wakati huu hakuna jibu , lakini swali linaendelea kubaki , Ujerumani itakuwaje baada ya uchaguzi, serikali ijayo itakuwaje itaundwa na vyama gani na mwelekeo gani itachukua. Swali hili hakuna anayeweza kulijibu , baina ya Merkel na martin Schulz na ni kwamba kila kitu kiko wazi , na mwishowe baadhi ya vyama vidogo ndio vitaamua ni aina gani ya serikali ya mseto itaundwa.
Baadhi ya watu wanazungumzia dhidi ya muungano uliopo sasa wa chama cha CDU na SPD, yaani muungano unaojulikana kama wa rangi nyeusi na nyekundu. Mhariri wa gazeti la Rhein-Neckar-Zeitung la mjini Heidelberg anazungumzia kuhusu muungano huo mkuu pamoja na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD.
Huenda basi chama cha AfD kingekuwa chama kikuu cha upinzani , kingepata haki ya kuzungumza bungeni kama sehemu ya serikali kivuli. Bila shaka wanainchi wa Ujerumani wangelazimika kukubaliana na hali hiyo. Lakini ni kutokana na kulazimika tu. Martin Schulz kutoka chama cha SPD awe kiongozi wa upinzani. Huo hautakuwa uchaguzi mbaya.
Mada nyingine ni kuhusu maafa yaliyosababisha na kimbunga Irma. Mhariri wa gazeti la Südwest-Presse la mjini Ulm anaandika:
Kiwango cha juu cha joto cha maji katika maeneo ya tropiki kinasababisha mabadiliko ya hali ya tabia nchi. Uharibifu mkubwa uliofanywa na kimbunga Harvey na Irma nchini Marekani ni matokeo ya kudharau mabadiliko hayo. Marekani inapaswa kujichunguza binafsi. Wamarekani wanapaswa kumfahamisha rais wao kwa utulivu kabisa, kwamba chungu kikichemka maji hutoka kupitia mvuke.
Gazeti la Aachener Nachrichten linazungumzia kuhusu michuano ya Champions League inayoanza rasmi leo kwa awamu ya makundi.
Michuano hiyo inaanza rasmi leo, lakini mhariri anaiangalia zaidi klabu ya Paris St. Germain ambayo imetumia fedha nyingi msimu huu kujiimarisha.
Mhariri anasema rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya Aleksander Ceferin hana tatizo na kuifungia klabu kama Paris St. Germain kucheza katika Champions League , lakini kuizuwia klabu hiyo ya Ufaransa inayopata fedha kutoka kwa masheikh wa ghuba kufanya mchezo wanaoucheza na klabu hiyo na kuzuwia mchezo wa mpira kuharibika hilo halitatokea. Klabu hiyo inayomilikiwa na masheikh kutoka Qatar watatoa hatimaye msaada kidogo kwa shirikisho hilo , halafu kila kitu kitakwenda kama kilivyo.
Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman