Wahariri wameandika Tunisia na kujiuzulu kwa Michael Flynn
15 Februari 2017«Badische Neueste Nachrichten»Likizungumzia Tunisia Mhariri anasema:
Inavyoonesha uhusiano wa siku za baadae kati ya mwenye kufadhili na mwenye kufadhiliwa utategemea umoja wa Ulaya kufuata muongozo uleule ambao umekuwa ukifikiriwa na hasa ikiwa Umoja wa Ulaya utataka kujenga vituo vya kuwapokea wakimbizi katika ardhi ya Tunisia.Kwahivi sasa ni wazi kwamba waziri mkuu wa Tunisia Youssef Chahid hataki kujuwa lolote juu ya fikra hiyo ingawa kinyume chake hata yeye binafsi anafahamu fika kwamba hawezi kutowa masharti.
Gazeti la «Freie Presse» Mhariri anasema kwamba kwa vyovyote vile wajerumani pia wanataka kwa maslahi yao kuona watu wa Afrika Kaskazini na nchi nyingine zenye uchumi dhaifu wakipatiwa msaada badala ya kuwanyima na kusababisha kushamiri makundi yanayofanya biashara ya kuwasafirisha watu kimagendo.Mhariri huyo anaendelea kusema. Daima Ujerumani inahamu ya kuwasaidia watu katika Afrika kaskazini pamoja na maeneo mengine yenye hali mbaya ya kiuchumi, ili kuwapa watu hao matumaini mema na kuondokana na umasikini. Kwa upande mwingine Ujerumani inaweza kwa msaada wake pia ikafanikisha matakwa yake kwa washirika wake na hilo ni suala muhimu. Na pia itaimarisha utaratibu wa kwanza kuwatambua uraia wao wahamiaji waliokataliwa na ikiwezekana kuwarudisha makwao na hasa ikiwa imetambuliwa kuwa ni kitisho cha ugaidi nchini.
«Mannheimer Morgen»Linazungumzia kujiuzulu kwa mshauri wa usalama wa ndani Marekani Michael Flynn
Kadhia ya kujiuzulu kwa Flynn iliyovunja rekodi imeiongezea tope sura ya rais Donald Trump ambayo kutokana na kuendelea na chuki zake dhidi ya waandishi wa habari waliobobea imesababisha azidi kumulikwa , lakini wakati huohuo kile ambacho ni vigumu kukipima ni kwamba Trump anajikuta akikabiliwa na maswali magumu bila ya kuwa na mshauri.Na kutokana na hilo anaonekana wazi kwamba hana lolote analolijua katika masuala ya usalama ni mtupu kabisa.Agenda ya sera ya usalama pia kwa mtawala huyo ni ya kubabaisha.Tayari dikteta wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameshaanza uchokozi kwa kufanya majaribio ya Roketi na leo agenda kubwa ni ujio wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu mjini Washington na hapo hapana shaka kwamba litakalojadiliwa miongoni mwa mengine ni makubaliano ya Nyuklia na Iran.Yote hayo kwa rais anahitaji kuwa na mshauri atakayemuongoza kuyashughulikia barabara masuala hayo ya sera ya usalama na bila ya kuwepo mshauri huyo, kila kitu kitaparaganyika.