Magazetini Ujerumani
17 Machi 2015Donakurier linasema hivi
Kashfa juu ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na waziri wa fedha wa Ujerumani wiki iliyopita sasa yamempa nafasi ya kunyoosha kidole waziri wa fedha wa Ugiriki Yanis Varoufakis.Na kwahivyo hilo limeweka kigezo cha kusisitiza sababu ya matatizo ya madeni ya nchi hiyo ya Ugiriki inayoelekea kufikilisika.Ni vigumu kwahivyo kutatua mvutano wa nchi hizi mbili.Na hasa kwakuwa wagiriki wanaungalia mgogoro huu ambao ni kitisho kwa nchi yao kama unatokana na historia kwasababu katika jukwaa la kisiasa malumbano kati ya wanasiasa vijana wa serikali ya Ugiriki na Waliobobea kiuchumi wa serikali ya Berlin na Umoja wa Ulaya mjini Brussels yanaendelea.
Mannheimer Morgen» Linasema Bado Ugiriki haijakuwa muflisi.Lakini mtu anaweza kupata hisia kwamba Ujerumani imeshatabiri nchi hiyo kufilisika.Neno baya lililotumiwa na waziri wa fedha Schauble ya kuitaja Ugiriki kuwa ni ''Graccident'' kwa namna yoyote halitotosaidia kutuliza hisia na hali ya mambo. Isipokuwa kuungoze nguvu tu mvutano kati ya serikali mjini Berlin na Athen ambao tayari ulishavuka mpaka tokea muda mrefu. Mhariri huyo anaendelea kusema kwamba Schauble na wenzake amezusha hisia za kuonekana kwamba ni ili uwe sawa Ulaya ni lazima ufuate njia ya Ujerumani.Lakini inawezekana pia Ugiriki katika msimamo wake mbele ya mahakama ya Kimataifa alau ikawa na haki ya kupata japo sehemu ya fedha zake inazoidai Ujerumani.
Katika suala la mkutano kati ya rais wa Ukraine na Kansela Angela Merkel mhariri wa gazeti la Nurnberger Zeitung ameandika kwamba
Rais Poroshenko anatia huruma kwa kiasi fulani. Na ni kwasababu pengine alitegemea mengi kutokana na ziara yake Ujerumani. Lakini kwa mra nyingine tena amevunjwa moyo na Kansela Merkel kwa kukataa kumpa silaha, sio hilo tu lakini pia ahadi za kupatiwa fedha zimesogezwa mbele. Juu ya hilo limekuja pia suala la utekelezaji wa makubaliano ya amani ya amani ya mjini Minsk limeibuka. Na hapo Poroshenko analazimika kumpa haki yake kansela Merkel kwa kulipa kipaumbele hilo. Vile vile kukubali kwamba suala la kuisusia michezo ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi haliwezi kutumiwa kuipa vitisho Urusi. Na hasa kwakuwa hilo la kutumia vitisho halijawahi kufanikiwa hata huko nyuma.
Kölnerstadt Anzeiger linasema katika hali rasmi Rais Poroshenko na kansela Angela Merkel ni watu wanaosifiana sana. Lakini huenda ikawa sio kila mmoja anakubaliana na hilo kwa hali zote kutokana na kilichojitokeza katika mkutano wa wawili hao mjini Berlin. Mhariri amesisitiza kwamba kinachodhihirika ni kwamba kuchafuana ni hali ya kawaida kuanzia Ukraine, Moscow, Brussels hadi Washington kwahivyo Kansela Merkel anabidi kuvumilia kughadhabishwa kwake. Ushawishi wake kwa Putin una kikomo chake. Na ushawishi wake kwa Poroshenko unabidi kuwa mkubwa zaidi. Mara zote amekuwa akiushinikiza utawala wa Moscow kuzingatia makubaliano ya Minsk lakini hilo halijafanikiwa.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed AbdulRahman